Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Wawakilishi wa Walii Faqih katika mikoa tofauti nchini humo, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu uliofanyika Tehran na baada ya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Irani pamoja na baadhi ya viongozi wa nchi, kwa kutoa tamko rasmi waliwataka wakuu wa mihimili mitatu ya dola (bunge,mahakama na serekali) kwa kupanga mipango thabiti, ugawaji bora wa rasilimali, mapambano makali dhidi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na upendeleo, pamoja na uangalizi endelevu wa utekelezaji wa sera za kiuchumi, wachukue hatua za vitendo za kupunguza shinikizo la maisha kwa wananchi, na waweke mbele kabisa kushughulikia hali ya makundi yaliyo hatarini, uundaji wa ajira endelevu, udhibiti wa mfumuko wa bei na kuboresha uwezo wa ununuzi wa wananchi.
Matini kamili ya tamko ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Kwa fadhila za Mola Mlezi na kwa msukumo wa kishujaa wa taifa lenye heshima la Iran, tukio la kihistoria la tarehe 12 January 2026, katika utetezi wa uadilifu wa ardhi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, lilidhihirika wazi. Tukio hili tukufu lilikuwa jibu kali kwa mlolongo wa njama tata za kambi ya ubeberu wa dunia, ikiongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni, zilizopangwa katika mfumo wa “vita kamili ya mseto”. Lengo la mwisho la mashambulizi haya yaliyoratibiwa lilikuwa ni kuwasha moto wa vita vya ndani, kutishia umoja wa kitaifa, kugawanya ardhi ya nchi na kuangamiza miundombinu muhimu ya taifa.
Ushindi huu mkubwa umetokana na neema za Mwenyezi Mungu na uangalizi wa Imamu wa Zama (roho zetu ziwe fidia kwake), uongozi wa hekima wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, upinzani wa kishujaa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, nguvu thabiti za jeshi la polisi na vyombo vya usalama, hususan wanajeshi wa kujitolea wa Basij walio tayari kujitoa muhanga, pamoja na ufahamu, busara na utambuzi wa wakati wa kipekee wa taifa la Iran, ambao katika mazingira magumu waliweza kutenganisha kwa uwazi maandamano ya madai halali na vurugu.
Sasa, kwa baraka ya damu safi ya mashahidi madhulumu walinzi wa usalama na kujitolea kwa majeruhi, ambapo shambulio kubwa na zito lisilo na mfano la kambi ya uadui kwa msaada wa Marekani na Uzayuni limekabiliwa na kushindwa, na utulivu kurejea nchini, sisi Wawakilishi wa Walii Faqih mikoani, ambao tuna heshima ya kulitumikia taifa lisilo na mfano la Iran, mwishoni mwa mkutano wetu wa majira ya baridi tunawasilisha hoja zifuatazo:
1. Rais mwongo, mhalifu na muuwaji wa Marekani pamoja na wapangaji sera wa Kizayuni katika Ikulu ya White House wanapaswa kujua kwamba aina yoyote ya dharau au shambulio dhidi ya heshima ya Imamu wa Umma wa Kiislamu haliwezi kutokea na limehukumiwa kushindwa bila shaka. Kitendo kama hicho kitawasha moto wa ghadhabu ya Umma wa Kiislamu katika eneo lote na kuunda wimbi kubwa litakaloangamiza uwepo wa utawala mchafu wa Kizayuni, na kuyaweka maslahi ya Marekani katika eneo lote na duniani kote kwenye tufani kali itokayo kwenye mataifa ya Kiislamu na taifa shujaa la Iran.
2. Tunatoa rambirambi za dhati kwa wananchi wetu wote wapendwa ambao kwa namna yoyote walidhurika katika fitna hii; iwe ni familia tukufu za mashahidi shujaa na madhulumu walinzi wa usalama, familia zilizoathirika zilizopoteza wapendwa wao kutokana na njama za mauaji ya magaidi, majeruhi, waliopata majeraha ya kimwili na kisaikolojia, pamoja na wananchi wapendwa ambao mali zao ziliharibiwa.
Kwa mujibu wa msisitizo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, vyombo vya mahakama na usalama vina wajibu wa kuzingatia kikamilifu misingi ya kisheria na ya Kiislamu, na kwa umakini, kutofautisha kati ya waandamanaji na wachochezi wa vurugu.
Aidha, inafaa kwamba wale waliodanganywa na hawakuhusika katika uhalifu uliopangwa, wachukuliwe kwa huruma ya Kiislamu na kwa mtazamo wa malezi, ili kuweka mazingira ya kurejea kwao katika jamii ya Kiislamu. Lakini kwa wahusika wakuu wa vita vya kigaidi vya hivi karibuni na wale waliopigana dhidi ya mfumo na usalama wa taifa, na ambao hukumu ya "muharib" inathibitika juu yao, matakwa ya wazi ya taifa ni utekelezaji wa haraka wa adhabu kali zaidi, baada ya uchunguzi wa haki na wa uwazi.
3. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa tamko lenye mshikamano na uwajibikaji la wakuu wa mihimili mitatu ya dola, lililoonesha sauti moja na mshikamano wa viongozi katika kuvuka awamu hii. Tunasisitiza kwamba hatua hii iwe mwanzo wa harakati mpya, ya ziada na ya kimapinduzi katika njia ya kuwahudumia wananchi.
Matarajio ya taifa ni kwamba mihimili ya utendaji, ya kutunga sheria na ya mahakama, kwa kuhamasisha uwezo wote wa kitaifa na kwa uongozi wa jihadi, itekeleze kikamilifu ahadi zilizotolewa. Kipaumbele na dharura ya sasa ni kuzingatia maisha ya wananchi na kutatua kwa vitendo matatizo ya kiuchumi. Kwa mipango thabiti, ugawaji bora wa rasilimali, mapambano makali dhidi ya rushwa, ubadhirifu na upendeleo, pamoja na uangalizi endelevu wa utekelezaji wa sera za kiuchumi, lazima zichukuliwe hatua za vitendo za kupunguza shinikizo la maisha kwa wananchi. Kushughulikia hali ya makundi yaliyo hatarini, kuunda ajira endelevu, kudhibiti mfumuko wa bei na kuboresha uwezo wa ununuzi wa wananchi lazima viwekwe mbele ya kila jambo.
Vilevile, inatarajiwa kwamba vyombo vya utendaji, kwa kuunda mifumo ya uwazi na uwajibikaji, kwa uwepo wa moja kwa moja katika maeneo mbalimbali ya nchi na kwa kusikiliza moja kwa moja kero za wananchi, vikubali kwa nia njema malalamiko na maandamano ya wananchi wetu wapendwa, na kuyajibu kwa njia ya busara na yenye kuleta suluhisho.
4. Kulengwa kwa makusudi kwa misikiti, vituo vya kidini na kuidharau Qur’ani Tukufu kumeondoa pazia na kufichua sura halisi ya wapangaji wa vurugu hizi, na kubainisha wazi mwelekeo wao wa kipagani na kibeberu. Vitendo hivi vya kikatili vimejaza nyoyo huzuni na majonzi, na kuumiza hisia za taifa lenye heshima la Iran. Hata hivyo, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa juhudi kubwa na misaada ya kujitolea ya wananchi waumini na wafadhili wema, ujenzi upya wa nyumba za Mwenyezi Mungu na za wananchi utafanyika kwa kasi na kwa ubora zaidi kuliko hapo awali.
5. Swala za Ijumaa kote nchini daima zimekuwa mstari wa mbele katika kudai haki na katika kuunganisha taifa na serikali, na zimecheza jukumu lao la kihistoria. Maimamu wa Swala ya Ijumaa, katika mwelekeo wa kukamilisha na kuboresha mifumo ya utoaji huduma, wako tayari kikamilifu kuweka mazingira mwafaka ya mazungumzo ya moja kwa moja, endelevu na ya pande mbili kati ya wananchi na viongozi, katika misikiti na viwanja vya Swala. Utekelezaji wa vitendo wa jambo hili unahitaji ushirikiano na azma ya dhati ya vyombo vyote vya utendaji, ili tushuhudie ukaribu mkubwa zaidi kati ya dola na taifa na kuimarika kwa imani ya umma.
InshaAllah, kwa baraka ya subira na ustahimilivu wa taifa kubwa la Iran, ushindi mkubwa zaidi na kuwashinda maadui wa Iran na wa kambi ya muqawama utakuwa ni fungu la wananchi wetu wenye subira na shukrani.
Kwa matumaini ya ushindi wa Umma mkubwa wa Uislamu, uhuru wa Quds, kudhoofika zaidi kwa Marekani mlafi wa dunia, na kuangamia kwa haraka zaidi kwa utawala wa Kizayuni unaoelekea kutoweka.
Na amani, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu
Wawakilishi wa Walii Faqih katika Mikoa ya Iran
Tehran – January 2026
Maoni yako